Proverbs 5:11-14

11Mwishoni mwa maisha yako utalia kwa uchungu,
wakati nyama na mwili wako vimechakaa.
12Utasema, “Tazama jinsi gani nilivyochukia adhabu!
Tazama jinsi moyo wangu ulivyodharau maonyo!
13Sikuwatii walimu wangu
wala kuwasikiliza wakufunzi wangu.
14 aNimefika ukingoni mwa maangamizi kabisa
katikati ya kusanyiko lote.”
Copyright information for SwhNEN